Sunday, August 10, 2014

Thursday, February 20, 2014

FIRST CRUSADE BAND


First crusade band ni bendi ya muziki wa injili ambayo imeundwa na kikundi cha wanafunzi wa chuo kikuu cha  Mwenge University College kilichopo mkoani Kilimanjaro, chini ya kikundi cha wanafunzi walio okoka (CASFETA TAYOMI).

Bendi hii ilianza rasmi mnamo mwaka 2013 wanachama wa Casfeta Tayomi chuo kikuu cha Mwenge walipokuwa katika mkutano wa injili huku mpakani mwa Arusha na Kilimanjaro katika wilaya za Arumeru na Siha. Band hii ilianzishwa chini ya maono ya mwenyekiti wa bendi hii Manase S Daudi na kuwashirikisha wenzake. Manase aliwashirikisha wenzake ambao walikuwa katika kamati ya chakula kwenye mkutano huo. Kutokana na shughuli na umuhimu wa kamati hiyo katika mkutano, hii ilikuwa ni sehemu yao ya utumishi pia, kwani ilikuwa ngumu kwao kwenda kushuhudia kwenye vijiji n ahata kushiriki kikamilifu katika mkutano.
Mpaka hibvi sasa First Crusade Band (FCB) inaundwa na watumishi watano ambao ni Manase Daudi, Josephine Daniel, John Steven, Helman Kilunga, Leah na Philip Mdoe.